Malipo yako ya kwanza, bila code
Malipo ya PigaPay kwenye tovuti yako
Pokea matokeo ya malipo kwa usalama
Jaribu, kisha anza rasmi
Malipo yako ya kwanza, bila code
Pokea malipo leo kwa linki ya malipo au QR code. Huhitaji tovuti.
- Fungua akaunti yako ya bure kisha thibitisha code tutakayokutumia.
- Fungua Linki za Malipo kwenye dashibodi yako na ubofye Linki Mpya.
- Weka kiasi (au mwache mteja aandike) na maelezo mafupi.
- Ishiriki: tuma linki kwa WhatsApp au SMS, au chapisha QR code uweke dukani.
- Mteja analipa kwa simu kupitia M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money au HaloPesa, nawe unaona malipo kwenye dashibodi yako.
Malipo ya PigaPay kwenye tovuti yako
Mpeleke mteja wako kwenye ukurasa wa malipo wa PigaPay. PigaPay inaomba namba ya simu, inatuma ombi la malipo, inamruhusu kujaribu tena na kumrudisha kwenye tovuti yako.
- Tengeneza key ya majaribio kwenye dashibodi yako: API Keys, kisha Tengeneza key, aina Majaribio. Nakili key na siri ya webhook.
- Pakua maktaba ya PHP na uihifadhi pamoja na code yako.
- Tengeneza checkout mteja anapobofya Lipa kwenye tovuti yako:
$pigapay = new PigaPay\Client(getenv('PIGAPAY_KEY')); $checkout = $pigapay->createCheckout([ 'amount' => $order->total, 'reference' => 'ORDER-' . $order->id, 'success_url' => 'https://yourshop.co.tz/paid', 'cancel_url' => 'https://yourshop.co.tz/cart', ]); header('Location: ' . $checkout['url']); - Onyesha ukurasa wa shukrani kwenye success_url yako. Weka oda kuwa imelipwa kutoka kwenye webhook pekee (mwongozo unaofuata), si kutoka ukurasa huu.
Pokea matokeo ya malipo kwa usalama
PigaPay inatuma kila matokeo kwenye webhook URL yako, yakiwa yamesainiwa kwa siri ya webhook yako.
- Weka webhook URL yako kwenye key (API Keys, Hariri), mfano https://yourshop.co.tz/pigapay/webhook.
- Hakiki saini kwenye kila ombi na ujibu 200:
$event = PigaPay\Webhook::fromRequest(getenv('PIGAPAY_WEBHOOK_SECRET')); if ($event['event'] === 'payment.completed') { markOrderPaid($event['reference'], $event['event_id']); // once per event_id } http_response_code(200); - Bofya Tuma jaribio kwenye ukurasa wa API Keys: seva yako inapaswa kujibu 200.
- Umekosa moja? PigaPay inajaribu tena baada ya dakika 1, dakika 5, dakika 30, saa 2... na kuorodhesha kila utumaji kwenye ukurasa wa API Keys.
Jaribu, kisha anza rasmi
Kwa key ya majaribio hakuna pesa inayotumwa wala simu inayoguswa. Namba hizi zinatoa matokeo haya:
- 255700000001 inashindikana (salio halitoshi), 255700000002 inaghairiwa, 255700000003 inabaki ikisubiri; namba nyingine yoyote inakamilika.
- Pakia nyaraka za biashara yako (BRELA, TIN, NIDA) ili uweze kutoa pesa.
- Tengeneza key halisi yenye mipangilio ileile na IP ya seva yako kwenye IP zinazoruhusiwa.
- Badilisha key kwenye faili la mipangilio, kisha fanya malipo halisi madogo moja kuhakikisha.