Imesasishwa: 29 Oktoba 2026
1. Kulipa biashara kupitia PigaPay
PigaPay inafikisha malipo yako ya simu kwa biashara uliyoilipa. Bidhaa au huduma, na kurejesha pesa zake, ni jukumu la biashara hiyo.
- Kurejeshewa pesa ya oda, wasiliana na biashara kwanza. Jina na mawasiliano yake yako kwenye risiti yako ya PigaPay.
- Kama umelipa mara mbili au kiasi kisicho sahihi kwa makosa, wasiliana na biashara na PigaPay ukiwa na namba ya kumbukumbu ya malipo. Kama pesa bado haijatolewa na biashara, PigaPay inaweza kuirudisha kwenye namba ya simu iliyolipa.
- Kama hukupata bidhaa na biashara haijibu, iambie PigaPay ukiwa na namba ya kumbukumbu: tutawasiliana na biashara na tunaweza kusimamisha utoaji wake wa pesa wakati tunafuatilia.
2. Jinsi pesa inavyokurudia
- Pesa inarudishwa kwa simu kwenye namba iliyolipa, baada ya kuhakiki namba ya kumbukumbu ya malipo.
- Makato ya mtandao wa simu kwa kutuma pesa hiyo yanaweza kutozwa.
- Tafadhali omba ndani ya siku 30 tangu malipo, ili malipo yaweze kufuatiliwa.
3. Biashara kurudisha pesa kwa wateja wake
Biashara inayotaka kumrudishia mteja pesa inawasiliana na PigaPay ikiwa na namba ya kumbukumbu ya malipo. Kiasi kinakatwa kutoka salio la PigaPay la biashara hiyo. Makato ya PigaPay kwa malipo yaliyokamilika hayarudishwi.
4. Ada za vifurushi vya PigaPay (wafanyabiashara)
- Kifurushi cha kulipia ni kwa mwezi au mwaka ulioouchagua. Unaweza kurudi kwenye kifurushi cha bure wakati wowote; muda uliobaki kwenye kifurushi cha kulipia haurudishwi kama pesa.
- Kama ulitozwa mara mbili au kwa makosa kwa kifurushi, wasiliana nasi ndani ya siku 30 na tutarudisha malipo ya ziada.
5. Mawasiliano
Simu au WhatsApp +255 678 520 538, barua pepe pay@pigatech.com, au ukurasa wa mawasiliano. Tafadhali weka namba ya kumbukumbu ya malipo.