Kuanza 6
Nafunguaje akaunti ya PigaPay?
Kuanza
Kufungua akaunti ya PigaPay ni rahisi na bure. Nenda ukurasa wa Anza Sasa , jaza taarifa za biashara yako, thibitisha barua pepe au namba ya simu, kisha unaanza kupokea malipo. Haichukui zaidi ya dakika 10.
Kuna majaribio ya bure?
Kuanza
Ndiyo! Kifurushi cha Starter ni bure kabisa, na unapata hadi miamala 100 kwa mwezi. Biashara ikikua, unaweza kupanda kwenda Business au Enterprise muda wowote.
Ninahitaji nini ili kuanza?
Kuanza
Utahitaji:
- Jina la biashara na taarifa za usajili
- Barua pepe na namba ya simu zinazofanya kazi
- Kitambulisho cha NIDA
- Namba ya TIN
- Akaunti ya benki au namba ya pesa kwa simu ya biashara
Mna app ya simu?
Kuanza
Bado. Dashibodi ya PigaPay inafanya kazi kwenye kivinjari cha simu yoyote: unaweza kuomba malipo, kufuatilia malipo na kutoa pesa ukiwa popote. Kidokezo: ifungue kwenye Chrome na uchague "Add to Home screen" ili ifunguke kama app.
Naweza kutumia PigaPay kwa malipo yangu binafsi?
Kuanza
PigaPay imetengenezwa hasa kwa biashara. Lakini hata mtu binafsi, mfano anayefanya kazi za kujitegemea au huduma ndogo, anaweza kuitumia kupokea malipo.
Nahakikije akaunti yangu?
Kuanza
Unathibitisha akaunti wakati wa kujisajili: tunakutumia code kwa barua pepe na SMS. Baadaye, ili uweze kutoa pesa, utapakia nyaraka za biashara (BRELA, TIN na NIDA) tuzihakiki.
Malipo 5
Pesa inaingia baada ya muda gani?
Malipo
Malipo ya simu yanathibitishwa ndani ya sekunde chache baada ya mteja kuweka PIN, nawe unayaona kwenye dashibodi yako papo hapo. Pesa inaweza kutolewa siku 0 baada ya malipo kukamilika. Utoaji wa pesa kwenda namba yako ya simu au akaunti ya benki unakaguliwa na timu yetu, kisha unatumwa.
Mnapokea sarafu gani?
Malipo
Shilingi za Tanzania (TZS). Wateja wanalipa kwa TZS kutoka pochi zao za pesa kwa simu, na salio lako na utoaji wa pesa ni kwa TZS.
Mnapokea mitandao gani ya simu?
Malipo
Mitandao yote minne ya Tanzania:
- M-Pesa (Vodacom)
- Mixx by Yas (zamani Tigo Pesa)
- Airtel Money
- HaloPesa (Halotel)
Natengenezaje linki ya malipo?
Malipo
Ingia kwenye akaunti yako, nenda "Linki za Malipo", weka kiasi na maelezo, kisha bonyeza "Tengeneza Linki". Nakili linki au pakua QR code, umtumie mteja kwa WhatsApp, SMS au barua pepe.
Je, wateja wanaweza kulipa kwa kadi au benki?
Malipo
Bado. Leo wateja wanalipa kwa pesa kwa simu (M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money na HaloPesa). Malipo ya kadi na benki yako kwenye mpango na yatatangazwa kwenye ukurasa wa Mabadiliko.
Mapya
Mapya
Usalama 4
PigaPay ni salama?
Usalama
Ndiyo. Kila ukurasa na ombi la API linatumia muunganisho uliosimbwa (HTTPS). Nenosiri zinahifadhiwa kwa njia isiyorudishwa, API keys zinahifadhiwa kama alama na zinaonyeshwa mara moja tu, na webhook zinasainiwa ili mfumo wako uhakiki zinatoka PigaPay. Akaunti zinafungwa baada ya nenosiri kukosewa mara kadhaa, na unaweza kuwasha kuingia kwa hatua mbili. PigaPay haioni PIN ya wateja wako: wanaiweka kwenye simu zao.
Mnajilinda vipi dhidi ya utapeli?
Usalama
Kila biashara inathibitishwa kwa usajili wake (BRELA), TIN na NIDA kabla ya kutoa pesa, na utoaji wa pesa unakaguliwa na timu yetu. Malipo kwenda akaunti ambayo biashara haijawahi kulipwa kwake yanasubiri saa 24 na mmiliki anajulishwa. Kuingia na API keys vina kikomo na vinafungwa baada ya kukosewa mara kadhaa. Ukiona malipo ya kutia shaka, tupigie au tuandikie WhatsApp mara moja.
Mna ulinzi wa hatua mbili (2FA)?
Usalama
Ndiyo. Kwenye Wasifu Wangu unaweza kuwasha kuingia kwa hatua mbili kwa app ya uthibitisho (Google Authenticator, Microsoft Authenticator, Authy na nyinginezo). Pia unapata code 10 za akiba endapo utapoteza simu.
Taarifa zangu zinalindwaje?
Usalama
Tunalinda taarifa zako kwa umakini. Taarifa zako zinahifadhiwa kwa usalama na hatumpi mtu mwingine bila ruhusa yako. Soma Sera ya Faragha kwa maelezo zaidi.
Bei na Malipo ya Kifurushi 4
PigaPay ni bei gani?
Bei na Malipo ya Kifurushi
Kifurushi cha Starter ni bure na kinajumuisha hadi malipo 100 kwa mwezi. Business na Enterprise vinaruhusu malipo zaidi na vinalipiwa kila mwezi au kila mwaka kwa pesa kwa simu. Ukurasa wa Bei unaonyesha bei na vikomo vya sasa.
Ona bei
Ona bei
Kuna makato kwenye kila muamala?
Bei na Malipo ya Kifurushi
Ndiyo: 2.85% + TSh 49.98 ya kila malipo yaliyokamilika, sawa kwa kila kifurushi. Malipo yaliyoshindikana au kughairiwa hayana gharama. Kwenye Mipangilio > Ada ya muamala unachagua nani anailipa: wewe, mteja wako, au nyote wawili (kugawana).
Naweza kusitisha kifurushi changu?
Bei na Malipo ya Kifurushi
Ndiyo. Vifurushi vya kulipia havijirudii vyenyewe: muda uliolipiwa ukiisha unarudi kwenye kifurushi cha bure cha Starter usipolipa tena. Pia unaweza kuhamia Starter wakati wowote kwenye ukurasa wa Kifurushi; muda uliobaki haurudishwi kama pesa.
Kuna punguzo ukilipa kwa mwaka?
Bei na Malipo ya Kifurushi
Ndiyo. Kulipa kwa mwaka kunagharimu takriban 20% chini kuliko kulipa kila mwezi. Chagua Kila Mwaka unapolipia kifurushi kwenye ukurasa wa Kifurushi.
Msaada wa Kiufundi 4
Naunganishaje API ya PigaPay?
Msaada wa Kiufundi
Mwongozo wa API una mifano ya PHP, Node.js, Python na cURL, na kuna maktaba tayari ya PHP. Tengeneza key ya majaribio kwenye ukurasa wa API Keys na ujenge kwa usalama: malipo ya majaribio hayafiki simu. Njia rahisi ya kuanza ni ukurasa wa malipo: PigaPay inaomba namba na kumrudisha mteja kwenye tovuti yako.
Mwongozo wa API Maktaba ya PHP
Mwongozo wa API Maktaba ya PHP
Mnapatikana saa ngapi?
Msaada wa Kiufundi
Timu yetu inajibu Jumatatu hadi Ijumaa, saa 3 asubuhi hadi saa 11 jioni (saa za Afrika Mashariki) kwa simu, WhatsApp, barua pepe na tiketi za msaada kwenye dashibodi yako. PigaPay yenyewe inafanya kazi saa 24 kila siku, na msaidizi wa mazungumzo kwenye tovuti hii anaweza kusaidia wakati wowote.
Najuaje kama mfumo unafanya kazi?
Msaada wa Kiufundi
Ukurasa wa Hali ya Mfumo unaonyesha kama tovuti, API na mitandao ya pesa kwa simu inafanya kazi, na unakagua tena kila dakika.
Hali ya Mfumo
Hali ya Mfumo
Naripotije tatizo?
Msaada wa Kiufundi
Fungua tiketi ya msaada kutoka Msaada kwenye dashibodi yako, au tutumie barua pepe. Tafadhali eleza ulichofanya, ulichotarajia, picha ya skrini na namba ya kumbukumbu ya malipo kama ipo. Tunajibu haraka iwezekanavyo siku za kazi.
pay@pigatech.com
pay@pigatech.com
Hakuna matokeo
Jaribu maneno mengine au angalia makundi hapa chini.